Mama Mmoja na Watoto 6 Wachanga Wanafariki kila Saa 2 ndani ya Yemen!

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

(Imetafsiriwa)

Licha ya majanga makubwa ya kibinadamu ndani ya Yemen kutokana na vita vilivyopelekea umasikini, ukame, kipindupindu, ukosefu wa huduma za afya na kusambaratika kwa kizazi chote, waamuzi katika usimamizi wa vita hivi wamefaulu japo kwa uchache kuweza kuwahadaa watu kuwa huu ni mzozo wa kindani katika eneo na kwamba unaendelea kuzidisha majanga ili kuweza kuwawekea pazia pande husika. Hii inaonyesha kiasi ya kutengwa na kutepetewa kwa suala la Yemen, ambalo limeingia mwaka wake wa nne katika “vita vya kimaslahi,” na imetoa kafara damu na maisha ya watu na mamilioni kufurushwa na wagonjwa kufikia kiwango cha kukata tamaa.

Yemen, Enyi Waislamu ni ardhi ambayo mama na watoto 6 wachanga wanafariki kila saa mbili kutokana na mimba na kujifungua kwa sababu ya ukosefu wa usimamizi wa afya, usafi, kuenea kwa maradhi, umasikini na ukame kwa kuwa ni nchi masikini katika Mashariki ya Kati!

Yemen, Enyi Waislamu inapakana na dola za Ghuba ambazo haziitambui kuwa ni sehemu ya GCC licha ya kwamba ina mzozo wa kimipaka na jirani Ufalme wa Saudi Arabia na Oman. Bali utiifu kwa Kafir Mmagharibi umeifanya Ufalme wa Saudi kwa maagizo ya Amerika kuongoza muungano wa kijeshi dhidi ya Yemen kwa kuivamia kijeshi pamoja na UAE, Oman na Qatar kabla ya kutolewa katika muungano huo! Watawala wa nchi hizo tulizozitaja na watawala wa Iran na watawala Yemen kaskazini na kusini wameshiriki katika kila aina ya uhalifu ambao umesibu watu wetu wa Yemen.

Yemen, Enyi Waislamu ni sehemu ya Ummah huu mmoja na tunaungana nayo kiAqeeda, kidamu, kicheo na kimatukufu na sio suala la kusahauliwa au kuzembewa hata kidogo, kiasi kwamba watu watazembea na kusahau janga lake na watu wake na kwa maisha ya watu wake, watoto, wanawake na wazee. Wakati huo huo majumba yanafunguliwa kwa ajiili ya mapaka na maumbwa duniani, mama na watoto sita wachanga wanakufa kila saa mbili ndani ya Yemen kutokana na njaa na maradhi. Je hili sio suala la kutia motisha wanaume na kuunganisha watu ili kutabban masuala ya Ummah na kuwaunganisha katika matatizo yao na kutafuta suluhisho lake?

Suluhisho la Yemen sio kwa kutafuta misaada ya kifedha kimataifa kama inavyopigiwa debe na UNICEF, mashirika ya misaada na Umoja wa Mataifa. Wamethibitisha dori yao ya kutiliwa shaka katika utekelezwaji wa ajenda za Kafir Mmagharibi. Ni aibu, kutamausha na kituko kuielekea Ulaya na Ikulu ya White House ili kuingilia kati na kupunguza janga hilo au kutangaza kuingilia kati kwa upole ili kusitisha janga hilo.

Ni fedheha kuona kwamba hayo ndiyo matakwa yetu ilhali Ummah wetu una majeshi ya kutosha na yenye uwezo wa kutatua suala la Yemen, Palestina, Syria, Iraq, Turkestan Mashariki, Myanmar na masuala mengine ya Ummah huu yakijumuishwa!!

Sisi sio Ummah usiokuwa na jeshi au utajiri kiasi kwamba tuweze kusimama mbele ya Magharibi na kuomba msaada na utajiri wao. Lau kuhodhi utajiri pasina mahitaji kumeharamishwa katika Uislamu na je kuhodhi silaha na majeshi ilhali tunayahitaji?! Majeshi haya yanabeba vyeo vikubwa duniani kinguvu za jeshi na wanaopigana kwa ujasiri na umahiri mkubwa lakini ni aibu kwamba yanashiriki katika uhalifu unaofanyiwa Yemen.

Janga la vifo vya kina mama na watoto wachanga kutokana na vita, umasikini, ukame, kipindupindu, ukosefu wa makaazi, kufurushwa na kila msiba ambao umeathiri watu wa Yemen unaweza kusuluhishwa kwa kutumia nguvu na ulinzi ambao utawalinda na kuwahifadhi wao kutokana na uovu kupitia jeshi kubwa ambalo litaokoa damu, hadhi, matukufu na kueneza amani, usalama na utulivu ndani ya dola kubwa na yenye nguvu! Hii ni Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume, ambayo Hizb ut Tahrir inafanya kazi kwa ajili yake.

Yemen, Enyi Waislamu ni moja katika kadhia za Ummah huu na hatutakiwi kuipuza na kuisahau, kwa kisingizio cha misiba mingi inayotuzunguka kwani Waislamu ni Ummah mmoja tofauti na watu wengine na Mtume (saw) alisema:

«إِذَا مَرَّ بِكُمْ أَهْلُ الْيَمَنِ يَسُوقُونَ نِسَاءَهُمْ، وَيَحْمِلُونَ أَبْنَاءَهُمْ عَلَى عَوَاتِقِهِمْ، فَإِنَّهُمْ مِنِّي، وَأَنَا مِنْهُمْ»

“Lau mutawaona watu wa Yemen mnapishana nao huku wakiwa na wake zao na wamebeba watoto wao katika mabega yao, basi wao wanatokana na mimi na Mimi ni miongoni mwao”

 

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

14 Shawwal 1440 Na: 1440 H / 035

Jumanne, 18 Juni 2019