Polisi Wanatekeleza Mauaji Ya Kutisha Chini Ya Vazi La Ugaidi

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la polisi limemuua mtu mmoja na watoto wake wawili kwenye uvamizi wa usiku katika Gatuzi la Kwale kusini mwa pwani ya Kenya. Polisi wanadai kwamba Mohamed Rahma Mapenzi  mwenye umri wa 41 anaejulikana pia kwa jina la Spanya, alikuwa gaidi anayewindwa na kwamba ati kwenye uvamizi huo aliwatumia watoto wake kama kinga dhidi ya risasi huku ikiwa akionekana kushika grenedi na kuwatupia maofisaa hao! Mke wa Marehemu bi Mwanahalima Mwachili aliekuwa na uja uzito wa miezi minane, alipigwa risasi tumboni na mguuni na sasa amelazwa kwenye hospitali ya rufaa ya Msambweni akiwa ana hali ngumu. Hizb ut-Tahrir Kenya, inatuma rambirambi zake za dhati kwa familia na marafiki wa marehemu na kumoumbea majeruhi afueni ya haraka.

Kufuatana ni kitendo hiki cha kikatili tunapenda kueleza yafuatayo:

Tokea kupitishwa kwa kanuni za kupambana na ugaidi, ni bayana kuwa maofisaa wa usalama wamekuwa wakiteleza mauaji ya watu kila mara pasi na uchunguzi wa kina wa washukiwa, bali kinyume cha amri ya mahakama. Polisi wamekuwa wakivamia majumba ya washukiwa, wakiwapandikizia silaha, hatimaye kuwauwa. Vipi polisi waliopokea mafunzo wadai kwamba baba wa damu alitumia watoto wake kama kinga kwake dhidi ya risasi?

Ni wakati raia wote na hasa jamii ya Kiislamu nchini kuisuta na kuikosoa hulka hii ya jeshi la polisi na kattu mauaji yao haya yanayotekelezwa chini ya jina la kupambana na ugaidi katu hayafai kufichwa chini ya mkeka. Ama wanasiasa wanaokuja kukashifu ukatili huu, hili kihakika si lolote lile ispokuwa huwa wanafanya hivyo kama mawakala tu wa kiserikali wa mahusiano ya umma.

Tunaeleza bayana kwamba udhalilishaji na unyanyasaji huu unaoshuhudiwa leo ni miongoni mwa maonevu mengi yanayofanyiwa Waislamu kote duniani, na kwa yakini  kamwe hayatokoma hadi pale Waislamu waanze kufanya kazi  kubwa inayolenga kusimamisha tena Khilafah- Ar-Raashidah  juu ya mfumo wa utume katika moja ya taifa kubwa la Kiislamu. Utawala huu ndio pekee ulio na uwezo wa kulinda Waislamu na hata wasokuwa Waislamu dhidi ya unyama wa aina yoyote ule.

 

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir in Kenya

 

REF: 1441/11 AH

Jumapili, 09th Shawwal 1441 AH/

31/05/2020 CE